KUSAMEHE NA KUSAHAU
Luk 17:3-4 Kisha Petro akamwendea Yesu akamwambia ‘Ndugu yangu anikose mara ngapi nimsamehe? Hata mara saba? Kutosamehe kunachafua roho yako, unaweza kuikosa Mbingu au Baraka za Mungu. Malaika ni wajumbe, watumishi wa Mungu wanapotumwa kwako kukuletea mahitaji mbali mbali sababu wenyewe wapo katika roho wanapo kuja wanaiona roho yako imechafuka basi wanarudisha kile kitu walichokuletea wanaenda kukihifadhi kinakaa kilipotolewa, kwa duniani hifadhi hizo tungeweza kuiita kabati, friji, store mpaka utakapo kaa sawa sawa etc. Mungu hawasikilizi wenye dhambi maombi ( Yoh mt 9:31 ) , sifa zao kwa Mungu huonekana kama ni makelele. Migogoro mingi katika ndoa chanzo kikubwa ni kutosameana Mume, mke, mtoto mabubu mhhhhh.Kunyimana nyimana vitu vilivyo haki katika ndoa, kukomoana. Mwanamke& Mwanaume kunyemelewa na Shetani kuhusu kutafuta altenative ( Mpumbavu huamua fasta, madhara yakamkuta) Shetani anazunguka zunguka akitafuta mtu, mwanachama ajoin, mapepo nayo yanazunguka zunguka...