KUSAMEHE NA KUSAHAU
Luk 17:3-4 Kisha Petro akamwendea Yesu akamwambia ‘Ndugu
yangu anikose mara ngapi nimsamehe? Hata mara saba?
Kutosamehe kunachafua roho yako, unaweza kuikosa Mbingu au
Baraka za Mungu.
Malaika ni wajumbe, watumishi wa Mungu wanapotumwa kwako
kukuletea mahitaji mbali mbali sababu wenyewe wapo katika roho wanapo kuja wanaiona
roho yako imechafuka basi wanarudisha kile kitu walichokuletea wanaenda
kukihifadhi kinakaa kilipotolewa, kwa duniani hifadhi hizo tungeweza kuiita
kabati, friji, store mpaka utakapo kaa sawa sawa etc.
Mungu hawasikilizi wenye dhambi maombi (Yoh mt 9:31) , sifa zao kwa Mungu huonekana kama ni makelele.
Migogoro mingi katika ndoa chanzo kikubwa ni kutosameana
Mume, mke, mtoto mabubu mhhhhh.Kunyimana nyimana vitu vilivyo haki katika ndoa,
kukomoana. Mwanamke& Mwanaume kunyemelewa na Shetani kuhusu kutafuta
altenative ( Mpumbavu huamua fasta, madhara yakamkuta) Shetani anazunguka
zunguka akitafuta mtu, mwanachama ajoin, mapepo nayo yanazunguka zunguka hayalali. (1Pet 5:8)
Mit. 17: 22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri;Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
Baadhi ya Matatizo/ athari anazoweza kupata mtu aliyena roho ya
kutosamehe/Uchungu wa Moyoni
Mioyo yetu haikuumbwa ikae na uchungu,
hasira, chuki. Ukikaribisha vitu hivyo unakaribisha Magonjwa, k.v. Presha, Kichwa Kuuma, Vidonda vya
Tumbo, Kuchanganyikiwa (Kuongea
Peke yako), Ajari, Asilimia kubwa ya watu wanojinyonga, kunywa sumu ni watu
walioumizwa na uchungu uliopitiliza
(Yuda Iskariote Mt 27:5), Watu wengine wamekasirika
wakaijikuta wapo Kifungoni wanajuta.Petro hakuwekeza kosa alilotenda la kumkana
Yesu tena mara 3 alitubu nakuomba msamaha, Akasamehewa.
Sala Ya Bwana Tunakiri kuwa “Baba yetu uliye
Mbinguni, utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe Waliotukosea”
Tunajifunga kwa maneno ya kinywa chetu wenyewe. Kama hutaki kusamehe na
kuachilia na Mungu naye hakusamehi ng’o nani anayeweza kuishi bila msaada wa
Mungu, bila ulinzi wake, upendo wake, neema yake? Ukihukumiwa kwa kosa hilo
siku ya siku ni haki yako sababu umekiri kwa kinywa chako mwenyewe.
Tuwe wepesi wa kuomba msamaha kwa Mungu wetu,
wenzi wetu hata watoto wetu
Katika wanafunzi aliokuwa nao Yesu Yuda alimsaliti Yesu
akakaa na uchungu hakuutoa ukamdhuru , Petro naye alimsaliti Yesu tena mara tatu.
Yuda mara moja, Petro mara tatu akatubu fasta. Akapata msamaha, sio suala la
dhambi kubwa au ndogo Mungu kwake hata dhambi iwe nyekundu husamehe kabisa.
Stephano Alipigwa na vijana waliofundishwa
na Sauli Stephano” Alikufa huku akiomba Bwana Usiwahesabiae Dhambi hii,
wasamehe Bwana.
Bwana Yesu pamoja na kudhalilishwa yeye
akiwa kama Mwana wa Mungu alikuwa na Jeshi kubwa la Malaika ambalo angeweza
kuliamlisha lifanye vyovyote, likafanya alidhalilishwa lakini akasema, Bwana
wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo.
Eliya alifanyaje
? Kama Eliya aliweza kuagiza moto kutoka Mbinguni uteketeze 50 Yesu si Zaidi!
Eliya Mtu wa Mungu kama mimi, kama wewe tu. Aliweza Yesu JE ! 2 Wafalme 1:10
Kutoomba Toba na kiburi mbele za Mungu au wanadamu,
maandiko yanasema Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.
Sio kwa sababu maandiko yanasema Samehe saba mara sabini
basi ndo iwe tiketi ya wewe kukosea kwa makusudi
, sababu utasamehewa kwa hiyo ukaamua kuleta Makwazo ya makusudi. Maandiko yana
onya juu ya mtu kama huyo alitaye makwazo. Pia sio kwa sababu Mungu ni wa
huruma au anasemehe si mwingi wa hasira, tusijiachilie sana tuwe na taadhali.
Luka
17. 1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo
hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!
Waefeso 4:26-27 '' Mwe na hasira, ila
msitende dhambi; jua lisichwe na ...
Shetani hawezi kukushambulia mpaka umfunguliae Mlango
hasira ni Mlango mmojawapo anaotumia
Kisasi ni cha Mungu, yeye atalipa tena walkati mwingine
Mungu hulipa tangia hapa duniani, Duniani tunapita hatuishi milele
Abigaili, mwanamke mwenye hekima wa Israeli
la kale, anatuwekea kielelezo kinachoonyesha matokeo ya kuomba msamaha, ingawa
aliomba msamaha kwa kosa la mumewe. Alipokuwa akiishi nyikani pamoja na
watumishi wake, Daudi, aliyekuja kuwa mfalme wa Israeli, alilinda kondoo za
Nabali, mume wa Abigaili. Hata hivyo, wakati vijana hao wa Daudi walipoomba
mkate na maji, Nabali aliwafukuza na kuwatusi vibaya sana. Daudi alikasirika na
kuongoza wanaume 400 hivi kwenda kumpiga Nabali na nyumba yake. Alipojua habari
hiyo, Abigaili alifunga safari kwenda kumlaki Daudi. Alipomwona, Abigaili
alimwangukia miguuni pake na kusema: “Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na
uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize
maneno ya mjakazi wako.” Kisha Abigaili akaeleza hali ilivyokuwa na kumpa Daudi
zawadi ya chakula na maji. Ndipo Daudi akamwambia: “Haya! Kwea kwa amani kwenda
nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako.”—1 Samweli 25:2-35.
Baada ya siku 10 Nabali alifariki, alivyofariki Daudi alifanya mpango wa kumuoa
Abigaili (Malipo ni hapa hapa Duniani)
Solomoni Mukubwa
(Ushuhuda)
Yeye ni Raia wa Kongo anayeishi Kenya ni mtoto wa kwanza
katika familia yao baba yao alipoongeza mke mwingine Huyo mke Mwingine alimloga
Solomoni Mukubwa alipokuwa na umli wa Miaka 12 akawa na uvimbe ambao ulipelekea
kukatwa kwa mkono wake ili kunusuru uhai wake, aliangaikiwa sehemu nyingi na
wazazi wake bila mafanikio. Alijua kuwa amelogwa na mama yake wa kambo baada ya
yeye mwenyewe kukiri kuwa alifanya hivyo. Huyu mama wa kambo naye aliokoka
baada ya yeye naye kupata pigo ‘Mwanawe alirukiwa na kijiti cha moto jichoni
kilichopelekea jicho la mwanawe kuharibika kabisa
(Malipo ni hapa hapa Duniani) ameimba wimbo unaitwa nimewasamehe !!!
Usipende kuudhi watu ovyo ovyo watu wengine Wanampendeza
Mungu kiasi ambacho ukikorofishana nao Malaika wananunua ugomvi unashangaa tu,
unapata pigo hujui chanzo ni nini.Hata katika ufalme wa giza nao kama kuna
kufanana Fulani ukimfanyia kitu kibaya anayelindwa na majini unaweza kukuta
majini wanakushambulia hata kukuua kabisa.
Kaini na Habili
Kisa cha Kaini kumuua Habiri ni hasira, uchungu ambao haukutubiwa
Mwanzo 4:1-15
uchungu wote
na ghadhabu na hasira na
kelele na matukano yaondoke kwenu,
pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi,
wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.(Waefeso 4:31,32)
Barikiwa
Ni
Mimi E.T.M.OMARI
Comments
Post a Comment