MUNGU HAJAZAA WALA HAJAZALIWA !!!
Friday, January 10, 2014
Mungu wa Imani nyingine wasio wakristo ni kweli hajazaa, hajazaliwa hana uwezo wowote yupo yupo tu.
Yehova Mungu wa wakristo yeye amezaa aliutuma ujumbe kwa kumtumia malaika ili aende kwa Bikira Maria kumtaarifu (Luka Mt.1:26-27) Mwezi wa sita, Maraika Gabriel alitumwa na Mungu aende mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali Bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbali ya Daudi; na jina lake Bikira huyo ni Maria,kuwa atachukua mimba kwa uwezo wa kiungu ambao haijawahi kutokea hapa duniani na kwa sababu yeye ni Mungu ana uwezo wa kufanya jambo lolote anaweza kuamuru hata mawe yawe watoto ikatokea hivyo. Anaweza kuamuru mtu aliye hai akawa mfu au mtu mfu akawa hai na ikatokea hivyo. ( 1Kor 9: 20-22) Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi,ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria ) ili niwapate walio chini ya sheria kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria ,(si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo) ili niwapate hao wasio na sheria kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge.Nimekuwa hali zote kwa watu wote ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.Ukitaka kuwapata watoto inakubidi nawe ujifanye mtoto ili kuwapata watoto japo kidogo bila hivyo hutawapata ng’o, Ukitaka kuwapata wenye pesa inabidi nawe ufanane fanane nao japo kidogo bila hivyo hutawapata hata kidogo.Kama hukutaka Mungu amtumie mwanadamu aliyemwumba tena mwanamke tu ambaye anaonekana kama kiumbe dhaifu kwa baadhi ya watu ulitaka Mungu atumie kuku au mbuzi ili kufikisha ujumbe kwa wanadamu aliowaumba kwa kuwagharamia sana, je kuku au mbuzi angekubarika miongoni mwa jamii ya wanadamu? Ni nani angekubali kusikia na kutilia maanani ujumbe ambao ungetolewa na kuku au mbuzi? Tungeweza kukubari na kutii kile (ujumbe) ambao Mungu angeutoa kwa kutumia kuku au mbuzi? Na kutii, iwapo kama kwa kutumia binadamu tu mpaka leo watu wengi bado wanakejeli kwa namna mbali mbali ule ujumbe ambao Mungu aliutelemsha kwa kumtumia Yesu?
Hata hivyo Mungu hakulazimika kuangaika sana kumtafuta mtu arudi katika njia yake ila ni basi aliamua tu, Mungu kwetu sisi binadamu hufanya vile aonavyo kuwa sawa kwa mtazamo wake sisi ni binadamu tu hatupaswi kuhoji, kulalamika sana mambo atufanyiayo Mungu, vinginevyo huenda tukaonekana tuna pingana na mipango na maamuzi yake, sisi ni udongo tu mbele za Mungu, yeye ni mfinyanzi (Yer 18:5-6) Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda?asema Bwana. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.
Histolia ina kawaida ya kutufundisha wakati uliopo, uliopita na wakati ujao.Vitu vingine Mungu anavyovifanya kwa wanadamu hupita fahamu zetu hata uambiwe akiri hufika ukomo wa kufikiri.
BAADHI YA MAAJABU AMBAYO MUNGU ALIYAFANYA KATIKA DUNIA HII TUNAYOISHI SASA
· Aliigawa bahari ya Shamu watu wakapita kati kati yake (Zab 66:5-6)
· Mungu aliwahi amuru mwanamke wa miaka 90 azae mtoto ikafanyika hivyo (Mwanzo 21:2)
· Mungu aliwahi ruhusu punda mnyama aongee sauti ya kibinadamu kitu ambacho hakitegemewi kabisa (Hesabu 22:28-30)
· Mungu aliumba sayari,nyota ,mwezi, jua vingine vinavyo onekana ambavyo bado kugunduliwa na visivyo onekana.
· Mungu aliwahi kuiangamiza dunia yote kwa maji na kubakisha watu nane tu walio mpendeza moyo wake.(1Petro 3:20)
· Mungu aliwahi simamisha Jua/Dunia kwa muda (Yoshua 10:13)
· Mungu aliwahi kuingilia mawasiliano ya mtu na mtu wasielewane ili kusudi lake litimie.(Mwa 11:1-9)
· Mungu anaweza fanya mvua inyeshe katika nchi na mafuriko yakatokea, pia anaweza ruhusu mvua isinyeshe na kukatokea ukame katika nchi yoyote aitakayo yeye.(1Fal 18:1)
· Mungu anaweza kufanya muujiza wa samaki wawili na mikate mitano wakala zaidi ya watu 10,000 watu wakala wakashiba na kuisaza.(Yoh Mt 6:1-13)
· Mungu anaweza amuru jabari/jiwe kubwa litoe maji ikafanyika hivyo (Hesabu 20:8 -11)
· Mungu anaelewa lugha zote za hapa duniani, hata lugha za wanyama, ndege,miti, bahari ,wadudu etc (Zab 96::11-12), (Zab 98:7-8)
· Kwa uweza na nguvu zake anatawala milele yote kwa haki tena ni mtakatifu mno mfano wake duniani, mbinguni hakuna. (Zab 66:7)
· Mungu aliwahi kumfufua Yesu aliyekuwa amekufa, Lazaro naye alifufuliwa tena walikuwa walishaanza kuoza na kunuka (Mark 8:31)
· Alimgeuza jambazi sugu Paulo aliyekuwa akiitwa Saul kutoka katika ufalme wa giza na kumuingiza katika ufalme wa nuru yaani wa Yesu Kristo.(Mdo 9:1-22)
· Mungu huyo huyo anaweza kumtumia mtu mwingine unayemdhania kuwa hafai, taka taka, kafiri kukuletea habari za ukombozi wa roho yako ukikubari ni kwa faida yako na ukikataa pia ni kwa hasara ya nafsi yako (1Kor 1:27)
· Mungu aliwahi ruhusu ardhi ifunue kinywa na kufumba iwameze wale walio mkosea kitu ambacho ukifikiria kwa akiri ya kawaida akiingii akirini, unashindwa kuelewa kabisa.(Hes 26:10)
· Mungu ana uwezo wa kukuona wewe usimuone, pia ana uwezo wa kurekodi matendo yako yote mabaya na mema na kuyaweka katika CD yake ya ki ungu na kuyatumia kama ushahidi wa siku ile ya hukumu itakapo fika.Hata jiwe linaweza kutoa ushahidi kwa Mungu (Yoshua 24:27)
· Mungu ana uwezo wa kuruhusu ushirika wa mwanamke na mwanaume azaliwe mtoto, kwa nguvu na uwezo wake, pia anaweza ruhusu mwanamke azae bila ushirika wa mwanaume kama ilivyo kwa bikira Mariamu (Mathayo 1:23/ Isaya 7:14) Ni kamuujiza cha mtoto mbele za Mungu.Mamaye Yesu pia aliuliza litakuwaje jambo hili wakati sijui mume…? Malaika/Mungu baada ya kujieleza mwisho akasema hakuna jambo la kumshinda Mungu, pia maana yake ni Mungu anaweza kufanya lolote atakalo, hashindwi na lolote. Hapa inamaliza maswali yote ya inawezekanaje kuzaa bila mwanaume, kwa mwelewa.(Luka mt 1:34-38)
· Aliokoa na anaendelea kuokoa kila siku watu wa Imani zote ambao walikuwa hawamjui Yesu baada ya kuujua ukweli wa Wokovu (Waebrania 3:7-8)
· Mungu pia haimtishi iwapo idadi kubwa ya binadamu/watu wataamua kwa hiyari yao ku tomfuata Yesu jina litupasalo kuokolewa kwalo wenyewe na kumfuata mfalme wa anga Shetani na mwisho kuangamia katika moto wa jehanamu. (Mwa 9:3) Alishawahi kuiangamiza Dunia na kuua watu wote kwa Gharika na kubakisha watu nane tu, pamoja na watu kulia na kusaga meno haikusaidia.
· Mungu halali hasinzii akitulinda, pamoja na ukaidi wetu, wakati sisi binadamu hulala, husinzia, tunapolala adui ni rahisi kutuvamia ni ulinzi wa Mungu tu utupao uzima siku hadi siku (Zab 121:3-5) Ayu 1:7-10)
· Katika ulimwengu tunaoishi kuna nyota nyingi mabilioni kwa mabilioni lakini Mungu zote azijua tena kwa majina na idadi ya nywele za vichwa vyetu vyote inajulikana, binadamu duniani tupo wangapi?(Luk 12:7) (Zaburi 147:4)
· Mambo aliyofanya Mungu na anayotufanyia sisi binadamu ni mengi mno hayaandikiki katika karatasi yakatosha hayahesabiki (Yoh 21:25) ingawa Shetani kwa dharau zake kwa Mungu anashawishi binadamu wayaone yote aliyofanya Mungu ni maajabu saba ya dunia. Hakuna maajabu saba ya dunia kuna maajabu zaidi ya maelfu ya Mungu sio ya dunia ni ya Mungu Mtakatifu, unapotaja Mungu unakuwa umemsifu Mungu, unapotaja dunia unakuwa umemsifu mungu wa dunia.
· Mbingu ni kiti chake cha enzi, duniani ni mahali pa kuweka miguu, Ukuu wa Mungu umepita ufahamu wa binadamu (Isaya 66:1)
· Mungu mbingu hazikutoshi wala mbingu za mbingu. Ewe mwanadamu kwa akiri yako utamlinganisha na kitu gani, kama si kumwacha tu Mungu aitwe Mungu.(2Nyakati 6:18)
· Mungu akipa kila kiumbe chakula chake, ulimwenguni hapa kuna viumbe vingapi? (Zab 136:25) Unataka kumfananisha na nani hapa duniani? Na Rais yupi, tajiri yupi, mfalme yupi?
TUKIO LINALO TEGEMEA KUTOKEA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA HAPA DUNIANI
· Ujio wa Yesu Kristo mara hii itakuwa kwa nguvu si kinyonge kama alivyokuja hapo mwanzoni (Mathayo mt 24:27-30)
TUKIO LINALO ENDELEA KWA SASA HAPA DUNIANI
Roho Mtakatifu kufanya kazi/shughuli mbali mbali na kanisa lake kwa ajili ya kuliandaa, (Warumi 8:28) na kuepuka mitego/hila mbali mbali ya Ibilisi anayoipanga kwa watu wa wote mf. ajali, maafa mbali mbali.
Wewe unayepinga uzazi wa Bwana Yesu na kutangazia uma wa watu usiku na mchana unampinga Mungu Yupi? Kama Mungu wako hawezi kitu, usimsemee Mungu wa wengine, usimsemee Yehova. Kwanza habari za Yesu hujui hata a, e,i,o,u yake . Hivi uliona wapi mtu hajui topic ya somo husika akaandaa muhadhara ili awaambie watu kuhusu hilo somo? Hivi kweli kwa mtu mwenye ufahamu wake atathubutu kwenda kusikiliza hapo mahali, hapo itakuwa ni kipofu anamwongoza kipofu mwenzake , itatokeaje kwao? (Luk Mt 6:39)
Mitume karibia wote walitabiri kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa jinsi uzazi wake utakavyokuwa kwa jinsi ya ajabu, wewe ni nani hata upinge hayo, kama sio wale ambao biblia takatifu ilikwisha watabiri kuwa siku za mwisho kutatokea Manabii wa uongo. Sasa kwa taarifa yako endelea tena kwa bidii juhudi za kupotosha, ila nakutaadharisha isije ikatokea laana kwako nadhani utakuwa unapingana na mpango kamili wa Mungu wa wokovu kwa wanadamu wote, ambao Mungu Mtakatifu aliingia gharama. Tena kwa kujua au kutojua unashindana na Mungu muumbaji wa dunia hii wote watakao shindana na Mungu wasitegemee kupata ushindi ni kushindwa tu na laana itakayokuwa ikiwakalia wote na njama hizo za kupotosha zinazo fadhiliwa na mawakala wa shetani na wapinga kristo maana wapo wengi, na wataendelea kuongezeka.Na Shetani atakuruka siku ya siku maana hakukutuma ila umejituma mwenyewe atakucheka wakati ukiteswa na hukumu ya Mungu.
Huyo unayempinga ndiye atakaye kuja kuhukumu dunia hii na watu wote waliokufa na walio hai kutokana na matendo yao misahafu imeandika hivyo kwa kusoma na sio kwa kusomewa au kutafsiliwa na mwingine. Pamoja na kuwa ujio wa Yesu mara ya kwanza ilikuwa ya kinyonge sana, mara ya pili atakapokuja atakuja kwa nguvu kubwa itakayoifanya Dunia yote kupigwa na butwaa kufumba na kufumbua.
Shetani, mapepo yanamjua Mungu kuliko sisi binadamu kwa hiyo kwa kumjua Mungu huko hukutumia kuwapotosha binadamu tupotee mbali na uso wake na kuharibu uhusiano mzuri ambao Mungu anautaka toka kwa binadamu wote, Mungu hababaishwi na dini, hata Shetani naye ana dini, yeye anachojua ni mahusiano mazuri (Utakatifu)
Ili kuilewa biblia inabidi uwe mmoja wa kondoo ukiwa nje hutaelewa utaishia kubisha tu na biblia ina lugha yake mf. Harusi ya mwana kondoo,maji yaliyo hai, kuzaliwa mara ya pili n.k kilicho andikwa kimeandikwa, kuna lugha ya biblia ukiwa si muamini hutaelewa ngo, kama ilivyo kwa wanasheria wana lugha zao za kisheria, madaktari wana lugha zao ili kuelewa inabidi uingie ndani. Wachawi wana lugha zao ukiwa si mchawi utatoka kapa.Wahuni wa vijiweni wana lugha yao ili kuelewa lugha zao inakubidi uingie ndani ujifunze ndio utaelewa bila hivyo utatoka kapa.
Kwa kuwa uzazi wa Yesu ndio msingi wa wokovu wote ukimpinga mtoto Yesu uzao wake utakataa kila kitu kinachomuhusu yeye utapinga miujiza, wokovu, kusurubiwa, kufufuka kwake na hata kurudi tena mara ya pili kwake na kwa kujua au kutojua utakuwa unapingana na Mungu na hapo kusudi la shetani la kutuchonganisha na Mungu litakuwa limekamilika.Wote wanaopinga uzazi wa Yesu, nawatahadharisha kuwa hili jambo kama litakuwa limetoka kwa mwanadamu mtafanikiwa kulipinga ila ikiwa limetoka kwa Mungu hamtaweza kulipinga, sababu mtakuwa mnapingana na Mungu. mtakuwa mkijitafutia laana, mikosi na mabalaa kwenu na vizazi vyenu. (Matendo ya mitume 5:38-39) Pia Mungu hashindani na mwanadamu hata siku moja na hata milele (Mwanzo 6:3)
Kama una nia umepanga kupinga uzao wa Yesu endelea kupinga, wokovu wake pinga, ujio wake mara ya pili pinga, na uwepo wa mbingu na kuzimu kuwepo pinga, sababu hata maandiko yanasema maandiko hayapati shida na watu wa jinsi hiyo au vikundi vya watu wa namna hiyo kwani haviwezi kubadilisha hata nukta moja ya msahafu, pia na hukumu inawasubiri na inaweza kuanzia hapa hapa duniani, na shetani atakupinga maana yeye anamjua Yesu kwamba ni mwana wa Mungu aliye hai na ndiye atakaye kuja uhukumu ulimwengu tunaoishi sasa.Pia ujue ya kuwa aliyekupa pumzi ni Mungu huyo unayepinga mipango yake ya kumtafuta binadamu akae katika njia yake, pamoja na bidii ya shetani naye kutaka binadamu wasisikie habari njema za wokovu wakae hivyo hivyo. Injili itapenya tu kila mahali katika siku hizi za mwisho hakuna wa kuzuia mipango ya Mungu.
Ndio maana wengine wanaacha kutumia vitabu vya Imani zao wanatumia misahafu ya makafiri, kama fulani ni kafiri sio safi ni mchafu, hafai mbele za Mungu kwa nini utumie kitabu chake, soma chako au subiri usomewe na kutafsiliwa.Kama hutaki basi ujue na kuamini kuwa Mungu alizaa na anaweza kufanya jambo lolote hapa duniani sababu yeye anaweza yote na akiri za Mungu hazichunguziki, na hata akiri yetu sisi binadamu wote ni ndogo kumwelewa jinsi Mungu alivyo.
Kama utakuwa tayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.
Dar es salaam Tanzania
Comments
Post a Comment